‏ Zechariah 9:5-7

5 aAshkeloni ataona hili na kuogopa;
Gaza atagaagaa kwa maumivu makali,
pia Ekroni, kwa sababu
matumaini yake yatanyauka.
Gaza atampoteza mfalme wake
na Ashkeloni ataachwa pweke.
6 bWageni watakalia mji wa Ashdodi,
nami nitakatilia mbali kiburi cha Wafilisti.
7 cNitaondoa damu vinywani mwao,
chakula kile walichokatazwa kati ya meno yao.
Mabaki yao yatakuwa mali ya Mungu wetu,
nao watakuwa viongozi katika Yuda,
naye Ekroni atakuwa kama Wayebusi.
Copyright information for SwhNEN
The selected Bible will not be clickable as it does not support the Vocabulary feature. The vocabulary is available by hovering over the verse number.