‏ Mark 6:45-52

Yesu Atembea Juu Ya Maji

(Mathayo 14:22-33; Yohana 6:15-21)

45 aMara Yesu akawaambia wanafunzi wake waingie kwenye mashua watangulie kwenda Bethsaida, wakati yeye alikuwa akiwaaga wale makutano. 46 bBaada ya kuwaaga wale watu, akaenda mlimani kuomba.

47 cIlipofika jioni, ile mashua ilikuwa imefika katikati ya bahari, na Yesu alikuwa peke yake katika nchi kavu. 48 dAkawaona wanafunzi wake wanahangaika na kupiga makasia kwa nguvu, kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho. Wakati wa zamu ya nne ya usiku, Yesu akawaendea wanafunzi wake, akiwa anatembea juu ya maji. Alikuwa karibu kuwapita, 49 elakini walipomwona akitembea juu ya maji, wakadhani ni mzimu. Wakapiga yowe, 50 fkwa sababu wote walipomwona waliogopa.

Mara Yesu akasema nao, akawaambia, “Jipeni moyo! Ni mimi. Msiogope!”
51 gAkapanda ndani ya mashua nao, na ule upepo ukakoma! Wakashangaa kabisa, 52 hkwa kuwa walikuwa hawajaelewa kuhusu ile mikate. Mioyo yao ilikuwa migumu.

Copyright information for SwhNEN
The selected Bible will not be clickable as it does not support the Vocabulary feature. The vocabulary is available by hovering over the verse number.

Everyone uses cookies. We do too! Cookies are little bits of information stored on your computer which help us give you a better experience. You can find out more by reading the STEPBible cookie policy.