‏ Leviticus 24:1-4

Mafuta Na Mikate Mbele Za Bwana

1 Bwana akamwambia Mose, 2 a“Waagize Waisraeli wakuletee mafuta safi ya zeituni yaliyokamuliwa kwa ajili ya mwanga ili taa ziwe zinawaka daima. 3 bNje ya pazia la Ushuhuda ndani ya Hema la Kukutania, Aroni ataziwasha taa mbele za Bwana kuanzia jioni hadi asubuhi bila kuzima. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo. 4 cTaa zilizo juu ya kinara cha dhahabu safi mbele za Bwana lazima zihudumiwe daima.

Copyright information for SwhNEN
The selected Bible will not be clickable as it does not support the Vocabulary feature. The vocabulary is available by hovering over the verse number.