‏ Matthew 25:1-6

Mfano Wa Wanawali Kumi

1 a“Wakati huo, Ufalme wa Mbinguni utakuwa kama wanawali kumi waliochukua taa zao na kwenda kumlaki bwana arusi. 2 bWatano wao walikuwa wapumbavu na watano walikuwa wenye busara. 3Wale wapumbavu walichukua taa zao lakini hawakuchukua mafuta ya akiba, 4lakini wale wenye busara walichukua taa zao na mafuta ya akiba kwenye vyombo. 5 cBwana arusi alipokawia kuja wale wanawali wote wakasinzia na kulala.

6 d“Usiku wa manane pakawa na kelele: ‘Tazameni, huyu hapa bwana arusi! Tokeni nje mkamlaki!’

Copyright information for SwhKC