Matthew 16:6-11
6 aIsa akawaambia, “Jihadharini. Jilindeni na chachu ya Mafarisayo na ya Masadukayo.” 7Wakajadiliana wao kwa wao, wakisema, “Ni kwa sababu hatukuleta mikate.” 8 bIsa, akifahamu majadiliano yao, akauliza, “Enyi wa imani haba! Mbona mnajadiliana miongoni mwenu kuhusu kutokuwa na mikate? 9 cJe, bado hamwelewi? Je, hamkumbuki ile mikate mitano iliyolisha watu 5,000 na idadi ya vikapu vingapi vya mabaki mlivyokusanya? 10 dAu ile mikate saba iliyolisha watu 4,000 na idadi ya vikapu vingapi vya mabaki mlivyokusanya? 11Inakuwaje mnashindwa kuelewa kwamba nilikuwa sisemi nanyi habari za mikate? Jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.”
Copyright information for
SwhKC