Ezekiel 30:1-6
Maombolezo Kwa Ajili Ya Misri
1Neno la Bwana likanijia kusema: 2 a“Mwanadamu, toa unabii na useme: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “ ‘Ombolezeni ninyi na mseme,“Ole wa siku ile!”
3 bKwa kuwa siku ile imekaribia,
siku ya Bwana imekaribia,
siku ya mawingu,
siku ya maangamizi kwa mataifa.
4 cUpanga utakuja dhidi ya Misri,
nayo maumivu makuu yataijia Ethiopia.
Mauaji yatakapoangukia Misri,
utajiri wake utachukuliwa
na misingi yake itabomolewa.
5 dKushi ▼
▼ Kushi ndiyo Ethiopia.
na Putu, Ludi na Arabia yote, Libya ▼▼ Libya ndiyo Kubu.
na watu wa nchi ya Agano watauawa kwa upanga pamoja na Misri. 6 g“ ‘Hili ndilo Bwana asemalo: “ ‘Wale walioungana na Misri wataangukana kiburi cha nguvu zake kitashindwa.
Kutoka Migdoli hadi Aswani,
watauawa ndani yake kwa upanga,
asema Bwana Mwenyezi.
Copyright information for
SwhKC