‏ Ezekiel 24:3-8

3 aIambie nyumba hii ya kuasi fumbo, na uwaambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “ ‘Teleka sufuria jikoni; iteleke
na umimine maji ndani yake,

4 bWeka vipande vya nyama ndani yake,
vipande vyote vizuri,
vya paja na vya bega.
Ijaze hiyo sufuria kwa mifupa hii mizuri;

5 cchagua yule aliye bora wa kundi la kondoo.
Panga kuni chini ya sufuria kwa ajili ya mifupa;
chochea mpaka ichemke
na uitokose hiyo mifupa ndani yake.

6 d“ ‘Kwa kuwa hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “ ‘Ole wa mji umwagao damu,
ole wa sufuria ambayo sasa
ina ukoko ndani yake,
ambayo ukoko wake hautoki.
Kipakue kipande baada ya kipande,
bila kuvipigia kura.


7 e“ ‘Kwa kuwa damu aliyoimwaga ipo katikati yake:
huyo mwanamke aliimwaga
juu ya mwamba ulio wazi;
hakuimwaga kwenye ardhi,
ambako vumbi lingeifunika.

8 fKuchochea ghadhabu na kulipiza kisasi,
nimemwaga damu yake
juu ya mwamba ulio wazi,
ili isifunikwe.

Copyright information for SwhKC